JIHAN MOHIN ASHINDA TAJI YA MISS GRAND INTERNATIONAL 2026
Nihani aiheshimisha Tanzania

Mshiriki Jihan Mohin ameshinda taji la Miss Grand International 2026 katika mashindano yaliyofanyika nchini Thailand, Oktoba 10, 2026.
Ushindi huo umefanyika katika moja ya mashindano makubwa ya urembo duniani, yanayowakutanisha washiriki kutoka mataifa mbalimbali kushindania taji hilo la kimataifa.
Kwa mujibu wa taarifa za habari, Jihan Mohin Dimack ameweka historia kwa kuwa Mtanzania wa kwanza na mwanamke wa kwanza kutoka Afrika kutwaa taji hilo tangu kuanzishwa kwa mashindano hayo.
Ushindi wake unaifanya Tanzania kupata heshima kubwa katika jukwaa la kimataifa la mashindano ya urembo.




